Mapping Africa's

Isimila



Isimila ni eneo la Enzi ya Kale ya Mawe katika Mkoa wa Iringa nchini Tanzania. Uchimbaji kwenye eneo la kati la kipindi cha pleistocene uliibua zana kubwa za kukata, vikwaruzi vingi na zana chache kiuhalisia za kazi nzito. Kwa sababu ya aina ya kumbukumbu ya vitu vya mawe vya kale vilivyopatikana, imefasiriwa kama inawakilisha eneo la baadaye la Acheulean ambalo lilikuwa limekaliwa kwa muda mfupi sana. Kulingana na ulinganifu wa kimaumbile kati ya vitu vilivyogunduliwa kutoka Isimila na vile vya aporomoko ya Kalambo, eneo hilo lilikadiriwa kwa muda kuwa la kipindi cha karibia 60,000 B.P.

Je, Ulijua?

Vitu vya kale vilivyochimbuliwa huko Isimila vinachukuliwa kuwa kati ya vitu muhimu zaidi vya Enzi ya Mawe kuwahi kutambuliwa.

Sources
1. Hansen, C.L. and Keller, C.M. (1971), Environment and Activity Patterning at Isimila Korongo, Iringa. American Anthropologist[Link]
2. Miller, J. M., Werner, J. J., Biittner, K. M. and Willoughby, P. R. (2020). Fourteen Years of Archaeological and Heritage Research in the Iringa Region, Tanzania. African Archaeology Review [Link]