Mapping Africa's

Olduvai Gorge



Olduvai Gorge, eneo la Enzi ya Awali ya Mawe lililopo kaskazini mwa Tanzania, pasipo shaka ni mojawapo ya maeneo mashuhuri na muhimu zaidi ya kiakiolojia duniani, na limekuwa msaada mkuu katika ujifunzaji wa mabadiliko ya binadamu. Eneo lenyewe liko katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, upande wa kusini-mashariki mwa Serengeti. Vitalu kadhaa katika Korongo hili vimetoa mkusanyiko wa visukuku vya binadamu na vitu vya kumbukumbu ya kale ambavyo vinachukuliwa kuwa muhimu katika utafiti wa mabadiliko ya binadamu. Baada ya ugunduzi wa Mary na Louis Leakey wa fuvu la Zinjanthropus katika eneo la FLK mnamo 1959, Olduvai ilionekana kuwa Chimbuko la Binadamu. Kumbukumbu za kwanza za zana za mawe zinazohusishwa na mabaki ya visukuku vya kale zaidi kutoka Olduvai Gorge vimepewa jina la Kiwanda cha zana cha Oldowan (kiwanda cha zana za mawe cha awali kabisa kuwepo barani Afrika).

Je, Ulijua?

Mojawapo ya kisukuku cha awali kabisa cha fuvu la nyani kupatikana lilikuwa pale Olduvai Gorge. Fuvu hilo lina umri wa miaka milioni 25 na lipo katika nyani wa kundi la Prokonsuli.

Sources
1. 1. Yravedra, J., Rubio-Jara, S., Courtenay, L.A., Martos J.A. (2020). Mammal butchery by Homo erectus at the Lower Pleistocene Acheulean site of Juma’s korongo 2 (JK2), bed III, Olduvai Gorge, Tanzania. Quaternary Science Reviews [Link]
2. Eren, M.I., Durant, A.J., Prendergast, M., Mabulla, A.Z.P. (2014). Middle Stone Age archaeology at Olduvai Gorge, Tanzania. Quaternary International [Link]