Mapping Africa's

Pango la Kuumbi (Zanzibar)



Maana ya neno Kuumbi katika Kiswahili ni ‘ukumbi mkubwa’, maelezo mwafaka ya vyumba vikubwa vinavyofanana na sebule zilizoinuka ndani ya eneo la pango. Uchimbaji wa kiakiolojia uliofanywa katika pango la Kuumbi kati ya mwaka 2004 na 2005 uliibua zana kadhaa za Enzi ya Mawe na mabaki ya wanyama waliotumiwa na watu wawindaji na wavuvi. Mabaki haya yanajumuisha mifupa ya twiga, pundamilia, jamii za ng’ombe, nyani, nyoka na konokono wakubwa. Vigae kadhaa, shanga, na sarafu huelekeza kwenye ukweli kwamba aina fulani ya biashara ya kimataifa ilifanyika mwambaoni katika nyakati za kihistoria. Makazi katika eneo la pango hilo umekadiriwa kuwa mwaka 20,000 KK na ufugaji wa kuku na ng’ombe unasemekana ulianza katika eneo hili takriban milenia ya 4 KK.

Je, Ulijua?

Eneo la pango la Kuumbi inasemekana liligunduliwa “kimapenzi” na wapenzi wawili waliokuwa wakitafuta mahali pa kukaa na kuzungumza. Kwa miaka kadhaa, pango hilo limekuwa mahali pa ibada takatifu kwa wakaazi wa Jambiani na Makunduchi.

Sources
1. Horton, M. C. and Clark, C. M. (1985). Archaeological Survey of Zanzibar. Azania: Archaeological Research in Africa [Link]
2. Shipton, C., Roberts, P., Archer, W. et al. (2018). 78,000-year-old record of Middle and Later Stone Age innovation in an East African tropical forest. Nature Communications [Link]
3. Wynne-Jones S. & LaViolette A. J. (2017). The Swahili World. Routledge.