Yakiwa yapata kilomita takriban 300 kusini mwa Dar es Salaam kando kando ya pwani ya Tanzania, Magofu ya Kilwa Kisiwani yalikuwa na nafasi muhimu katika biashara iliyovuka Bahari ya Hindi katika mwambao wa Uswahilini. Kisiwa cha Kilwa ni eneoi la mji lililo kubwa zaidi kupita miji yote ya wafanyabiashara kwenye pwani ya Afrika Mashariki. Eneo hili likiwa la kati ya karne ya 5 na 15 BK, linachukuliwa kuwa bandari tajiri ambayo ilitumika kama kitovu cha biashara kati ya Bahari ya Hindi na maeneo ya ndani ya Afrika Mashariki. Wakati wa umaarufu wake, ilitumika kama kituo muhimu kwa wafanyabiashara wanaosafiri kutoka Mashariki ya Kati hadi pwani ya Uswahilini, ikiwa ni pamoja na visiwa vya Komoro na kaskazini mwa Madagaska, kwa madhumuni ya biashara. Kilwa Kisiwani pia ilitengeneza sarafu yake yenyewe katika karne ya 11 hadi 14.
Mnamo mwaka 1981, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara yalipigwa chapa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO World Heritage List chini ya Mkataba wa Urithi wa Dunia Ulio wa Thamani Bora Ulimwenguni. Mnamo mwaka wa 2014, eneo hilo liliwekwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia Ulio Hatarini kwa sababu ya kuharibika na kuoza kwa mali hiyo, ambayo imesababisha kuporomoka kwa miundo ya kihistoria na ya kiakiolojia iliyofanya eneo hilo kuchapishwa awali.
Msikiti Mkuu wa Kilwa Kisiwani ndio msikiti mkongwe zaidi ambao ungali unasimama katika pwani ya Afrika Mashariki.
Sources
1. Chittick, N.H. (1974). Kilwa: An Islamic Trading City on the East African Coast. Nairobi: British Institute in Eastern Africa
2. Horton M. C. & Clark C. M.(1985). Archaeological Survey of Zanzibar, Azania: Archaeological Research in Africa [Link]
3. Ichumbaki, E.B. and Mapunda, B.B. (2017). Challenges to the retention of the integrity of World Heritage Sites in Africa: the case of Kilwa Kisiwani and Songo Mnara, Tanzania. Azania: Archaeological Research in Africa [Link]
4. Sutton, J.E.G. (1998). Kilwa: a history of the ancient Swahili town with a guide to the monuments of Kilwa Kisiwani and adjacent islands. Azania: Archaeological Research in Africa
5. Trimingham, J. (1975). “The Arab geographers.” In East Africa and the Orient: Cultural Syntheses in Pre-Colonial Times, edited by N.H. Chittick and R. Rotberg, 115–146. London: Holmes and Meier
6. UNESCO World Heritage. “Ruins of Kilwa Kisiwani and Ruins of Songo Mnara” [Link]
7. Wynne-Jones, S. (2005). “Urbanization at Kilwa, Tanzania AD 800–1400.” PhD dissertation, University of Cambridge.