Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (pamoja na Visiwa vya Mafia, Pemba na Unguja) ni nchi ya Afrika Mashariki ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba (Km2) 947,300, ambapo takriban Km2 885,800 ni nchi kavu na Km2 61,500 ni maji. Ikiwa na ukanda wa pwani wa kilomita 1,424, hali ya hewa inatofautiana kutoka kwa kitropiki kando ya pwani ya Bahari ya Hindi hadi hali ya joto la wastani katika nyanda za juu. Kilele cha juu kabisa cha Tanzania kiuhalisia ndiyo sehemu ya juu kabisa barani Afrika: Mlima maarufu wa Kilimanjaro, ambao una kimo cha mita 5,895. Mandhari ina sifa ya tambarare kando ya pwani, tambarare za nyanda za juu maeneo ya katikati na nyanda za juu pande za kaskazini na kusini. Matumizi ya ardhi yanaainishwa kuwa kilimpo takriban 44%, misitu 37%, na 19% iliyobaki kuwa ya matumizi mengine.
Kwa mujibu wa chapisho la Ethnologue, Tanzania ina lugha hai 129, ambapo mbili katika hizo zimetoweka. Kiswahili na Kiingereza ni lugha rasmi za nchi.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina maeneo saba ya kiakiolojia na kiurithi ambayo yameorodheshwa kwenye tovuti ya Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO. Kati ya maeneo hayo saba, matatu (Vituo vya Sanaa ya Miamba Kondoa, Magofu ya Kilwa Kisiwani pamoja na Songo Mnara, na Mji Mkongwe wa Zanzibar) yaliandikwa katika kundi la urithi wa utamaduni; matatu (Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Hifadhi ya Selous na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti) katika kundi la urithi wa asili na moja (Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro) katika kundi la urithi mchanganyiko. Maeneo haya yanasimamiwa kwa pamoja na Makumbusho ya Kitaifa ya Tanzania na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale. Tanzania pia ina maeneo sita kwenye orodha pendekezwa ya sasa ya Urithi wa Dunia.
Bofya kwenye mkusanyo wa sanaa ulio hapa chini ili kujifunza zaidi kuhusu baadhi ya maeneo haya na urithi wa Tanzania.
Utafiti Nje ya Maabara Nchini Tanzania
Wafanyakazi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale walifanya mazoezi ya utafiti Oktoba 2022 ili kuweka msingi wa maeneo ya urithi wa ukweli Zanzibar. Timu hiyo ilitembelea kisiwa cha Tumbatu, Fukuchani, Mvuleni, Mkokotoni, Pango la Kuumbi, Mangapwani, Chwaka, Unguja Ukuu, Kizimkazi, na Mwanampambe.
Mnamo Februari 2023 na Machi 2024, wafanyakazi na wanafunzi wa uzamili wa Idara ya Akiolojia na Mafunzo ya Urithi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walikuwa katika utafiti wakipambanua ukweli wa mambo ya kiakiolojia ambayo yametambuliwa kupitia utambuzi wa mbali na modeli za kiubashiri. Timu ilitembelea mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, na Arusha kufanya tafiti za kiakiolojia, kuchora ramani za jamii za maeneo ya kiakiolojia na urithi, na kufanya mahojiano.
-
Kuchukua usomaji wa GPS ndani ya Msikiti Mkuu katika Kisiwa cha Tumbatu -
Magofu ya Msikiti Mkuu katika Kisiwa cha Tumbatu -
Wafanyakazi wa DoMA wakiwa na Dkt. Daryl Stump (Chuo Kikuu cha York) wakifanya utafiti wa kuvuka mipaka Unguja Ukuu -
Kupambanua ukweli wa maeneo katika mkoa wa Iringa nchini Tanzania -
Javern Sabas (mwanafunzi wa uzamili katika akiolojia) akikusanya kauri zilizotapakaa akiwa mkoani Ruvuma.