Mapping Africa's

Maeneo ya Sanaa za Miamba Kondoa



Wilaya ya Kondoa katikati mwa Tanzania ni maarufu kwa maeneo kadhaa ya sanaa ya miamba ambayo yamehusishwa na kazi tofauti tofauti za eneo hilo. Maeneo haya yametangazwa kuwa Mnara wa Kitaifa kwa Sheria ya Mambo ya Kale ya Tanzania na yalichapishwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia imwaka 2006. Yakiwa na takriban kilomita za mraba 2,336, maeneo hayo yana sifa ya uibukaji wa wawindaji na wafugaji, wachungi, na mila za sanaa ya miamba ya wazungumzaji wa lugha ya Kibantu (Bwasiri 2013). Ingawa mila hizi wakati mwingine hupatikana pamoja katika makazi mamoja, kila mila ina mtindo na maudhui yake ya kipekee na.

Michoro ya miamba ya wawindaji na wakusanyaji huko Kondoa inajumuisha zaidi michoro za wanadamu na wanyama. Hata hivyo, michoro ya wanyama wakati mwingine hupambwa kwa barakoa au mitindo ya nywele ya ajabu, shanga, na kofia za kichwani. Michoiro ya binadamu kwa upande mwingine inawakilishwa zaidi katika maumbile yenye kiuno kilichopinda na yenye viungo kama vile sikio na mkia. Tamaduni ya sanaa ya miamba ya wafugaji inahusisha uchoraji wa makundi makubwa ya ng’ombe na silaha kama vile mikuki na ngao na zaidi ni yenye rangi nyeusi na kijivu. Tamaduni ya sanaa ya miamba ya wazungumzaji wa lugha ya Kibantu inajumuisha zaidi aina ya upakaji rangi kwa vidole ikionyesha maumbo tofauti ya kijiometria yakijumuisha nukta, mistari, miraba na miduara. Maumbile mengine ya wanyama wanaotambulika kama vile tembo na swala pia ni ya kipekee katika utamaduni huu.

Je, Ulijua?

Kondoa inawakilisha mojawapo ya mikusanyo bora zaidi ulimwenguni ya sanaa ya miamba ya zamani za kale, ikiwa na makadirio ya picha 1,600 za kipekee za pango zilizoenea katika maeneo takriban 200.

Sources
1. Bwasiri, E.J. (2008). The management of indigenous living heritage in archaeological world heritage sites: a case study of Mongomi wa Kolo Rock Painting Site, Central Tanzania. Unpublished MA dissertation, University of Witwatersrand, South Africa.
2. Bwasiri, E.J. (2011). The implications of the management of indigenous living heritage: the case study of the Mongomi wa kolo rock paintings World Heritage Site, Central Tanzania. South African Archaeological Bulletin [Link]
3. Bwasiri, E.J. and Smith, B.W. (2015). The rock art of Kondoa District, Tanzania. Azania: Archaeological Research in Africa [Link]
4. UNESCO World Heritage. “Kondoa Rock-Art Sites” [Link]